Wananchi wa Mkoa wa Dodoma na maeneo ya jirani wamehimizwa
kujitokeza kwa wingi kesho, Juni 23, 2026, kushiriki kilele cha Maadhimisho ya
Wiki ya Utumishi wa Umma 2026 yanayofanyika katika Viwanja vya Chinangali Park
jijini Dodoma.
Aidha, ushiriki wao utasaidia kupata huduma mbalimbali
zinazotolewa na Serikali pamoja na kujionea mafanikio yaliyofikiwa katika sekta
ya utumishi wa umma.
Wito huo umetolewa na Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais –
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Regina Qwaray, baada ya
kutembelea mabanda ya maonesho ya Wizara na Taasisi za Umaa zinazoshiriki
maadhimisho hayo.
Mhe. Regina amesema maadhimisho hayo yamekuwa fursa muhimu
kwa wananchi kupata huduma za papo kwa papo, ushauri na elimu kuhusu majukumu
na huduma zinazotolewa na Serikali katika sekta mbalimbali.
Aidha, amezipongeza Wizara na Taasisi za Umma kwa juhudi
kubwa wanazoendelea kufanya katika kutoa huduma na elimu kwa wananchi kupitia
mabanda ya maonesho, hali ambayo imeongeza uelewa wa wananchi kuhusu huduma za
Serikali na namna ya kuzifikia kwa urahisi.
Kilele cha
Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma mwaka 2026 kitafanyika kesho, Juni 23, 2026.
Afisa kutoka Ofisi ya Rai,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Bw. Edwin Bilikundi, (wa pili
kutoka kushoto) akitoa maelezo kwa Naibu Waziri, wa Ofisi hiyo, Mhe. Regina
Qwaray (wa pili kutoka kulia) kuhusu huduma zinazotolewa na Ofisi hiyo katika
maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma leo Juni 22, 2026 katika viwanja vya
Chinangali Park Jijini Dodoma
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Regina Qwaray akizungumza
na Watumishi wa Wizara ya Ardhi mara baada ya kuwasili katika banda lao la
maonesho kuona huduma zinazoendelea kutolewa kwa Wananchi kwenye Maadhimisho ya
Wiki ya Utumishi wa Umma leo Juni 22, 2026 katika viwanja vya Chinangali Park
Jijini Dodoma
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Regina Qwaray akiwa
katika picha ya pamoja na Watumishi wa Shirika la Reli Tanzania (TRC) mara
baada ya kuwasili katika banda hilo la maonesho kuona huduma zinazoendelea
kutolewa kwa Wananchi kwenye Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma leo Juni
22, 2026 katika viwanja vya Chinangali Park Jijini Dodoma
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Regina Qwaray (wa pili kutoka kulia ) akifurahia jambo wakati alipokuwa akitembelea mabanda ya maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma inayofanyika katika viwanja vya chinangali Park Jijini Dodoma
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Regina Qwaray Naibu Waziri, Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Regina Qwaray akizungumza
na Watumishi wa Wizara ya Maliasili na Utalii mara baada ya kuwasili katika banda lao la
maonesho kuona huduma zinazoendelea kutolewa kwa Wananchi kwenye Maadhimisho ya
Wiki ya Utumishi wa Umma leo Juni 22, 2026 katika viwanja vya Chinangali Park
Jijini Dodoma
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Regina Qwaray Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Regina Qwaray akizungumza na Soko la Bidhaa Tanzania (TMX) mara baada ya kuwasili katika banda lao la maonesho kuona huduma zinazoendelea kutolewa kwa Wananchi kwenye Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma leo Juni 22, 2026 katika viwanja vya Chinangali Park Jijini Dodoma
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Regina Qwaray Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Regina Qwaray
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Regina Qwaray (kulia) akikabidhiwa zawadi na Mkurugenzi wa Ofisi ya Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa, Bw. Frimin M. Msiangi, kama ishara ya shukrani kwa Taasisi hiyo kwa kutembelea banda lao la maonesho katika Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma Jijini Dodoma
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Regina Qwaray akisaini kitabu cha wageni, mara baada ya kufika katika banda la maonesho la Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) wakati wa maonesho katika Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma Jijini Dodoma
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Regina Qwaray akipokea maelezo kuhusu huduma mbalimbali zinazoendelea kutolewa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) mara baada ya Naibu Waziri huyo kuwasili katika banda la maonesho la Taasisi hiyo Juni 22, 2026 katika viwanja vya Chinangali Park Jijini Dodoma
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Regina Qwaray akizungumza na Watumishi wa Bunge mara baada ya kuwasili katika banda lao la Maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma Jijini Ddoma